Facebook

banner image

HALI YA VENGU BADO TETE

GLADNESS MALLYA NA SHAKOOR JONGO, DAR ES SALAAM
HALI ya afya ya staa wa vichekesho nchini, Joseph Shamba ‘Vengu’ ni tete na habari zilizolifikia gazeti hili zinasema afya yake imekuwa ikibadilikabadilika.
Habari kutoka kwa chanzo chetu makini ambacho ni ndugu wa karibu na familia hiyo, kwa sharti la kutotajwa gazetini alisema, afya yake bado haijaimarika tangu aliporejea kutoka nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Appolo.
CHANZO KINATIRIRIKA
“Hili suala ni la kifamilia zaidi na linafanyika kwa siri sana, kwahiyo usinitaje mahali popote...kiukweli hali ya Vengu bado hairidhishi. Tangu amefika tumejitahidi sana kumfanyisha mazoezi kama tulivyoelekezwa na madaktari wake lakini wapi!
“Anaumwa na kwa kweli sisi kama wanandugu tumechanganyikiwa sana. Tumekaa vikao na kujadiliana, maana wengi tulikuwa tumependekeza arudishe tena Appolo aendelee na matibabu lakini wengine wamekataa.

HALI YA VENGU BADO TETE HALI YA VENGU BADO TETE Reviewed by Anonymous on 2:59 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.